Simba sports club ni mabingwa watetezi wa Vodacom premium league na msimu huu wa mwaka 2020/2021 wako njiani kutimiza ndoto yao ya kuwa mabingwa tena kwa mara nyingine, hii
ni baada ya kuchukua kombe la SIMBA SUPER CUP ambayo ni mara yake ya kwanza kuanzishwa hapa nchini Tanzania na barani Africa kwa ujumla.
Timu ya Simba ndiyo timu pekee hapa barani Africa kuandaa mashindano yake kwa kugharamikia na maandlizi yote kufanywa na timu iyo huku ikialika timu kubwa hapa barani Africa . Timu zilizoalikwa na Simba sports club kwenye mashindano ya SIMBA SUPER CUP, ni TP MAZEMBE ya Congo, AL HILAL ya Sudan pamoja na wenyeji SIMBA.
YANGA YAPIGWA PINI NA FIFA SAKATA LA TAMBWE.
Timu ya Dar es salaam Young Africa imefungiwa na FIFA baada ya mchezaji wao wa zamani Hamis Tambwe kulalamikia fifa kuwa timu yake hiyo ya zamani haikumlipa mshahara wake na pia haikumalizia pesa zake za usajili wa kuja kuichezea yanga.
Timu hiyo imefungiwa na FIFA kutokufanya usajili wa dirisha dogo na dirisha kuu kwa muda wa misimu mitatu mfululizo, Kwa upande wake Hamis Tambwe amesema yeye hana shida na waajiri wake hao wa zamani, kikubwa wamlipe pesa zake anazozidai.
Kwa upande wa uongozi wa timu ya YANGA wamesema kuwa watamlipa mchezaji huyo pesa zake anazozidai mara moja kwani HIYO ni PESA NDOGO sana kwa YANGA. Hayo yamesemwa na msemji mkuu wa timu ya yanga NUGAZ pia amewataka mashabiki wa timu ya yanga kushusha presha, wasiwe na wasi wasi na timu yao.
SIMBA SPORTS CLUB WAALIKWA BUNGENI HII LEO.
Uongozi wa simba pamoja na wachezaji wa timu hiyo wamealikwa bungeni hii leo jijini Dodoma , ikiwa pia ni maandalizi ya timu hiyo kujiandaa na
mchezo wa ligi kuu hiyo kesho kwenye dimba la Jamhuri jijini Dodoma.
LIVE KESHO SIMBA KUMENYANA NA DODOMA JIJI.
Timu ya simba imewasili salama jijini Dodoma tayari kwa mchezo wake dhidi ya Dodoma jiji , mchezo unaotarajiwa kupigwa pale majira ya saa kumi kamili jioni uwanja wa Jamuhuri.
SIMBA SUPER CUP YAPOKELEWA VIZURI BARANI AFRICA.
Ni jambo la furaha na njema kwa mashabiki wote wa simba hapa nchini Tanzania na nje ya Tanzania kupitia kwa uongozi wa timu ya simba kwa kufanya mashindano ya SIMBA SUPER CUP, mashindano hayo yalifanyika katika ardhi ya Tanzania, uwanja wa Taifa jijini dar es salaam, hivyo timu ya simba kuwa mfano wa kuigwa na timu zingine hapa barani Africa .
Mmiliki wa timu ya simba MO DEWJI aweka wazi nia na madhumuni ya mashindano ya Simba Super Cup, kuwa ni maandalizi ya kwenda kuchukua ubingwa msimu huu, pamoja na kufika mbali kwenye michuano ya club bingwa barani Africa.
Pia Dewji amewaomba mashabiki wa simba hapa nchini Tanzania na nje ya Tanzania kujitokeza kwa wingi kuipa timu yao support pindi wanapocheza uwanjani bila kujali chochote.
TIMU YA SIMBA KUFANYA MAZOEZI YA MARA YA MWISHO .
Timu ya simba kufanya mazoezi yao ya mara ya mwisho kuikabili Dodoma jiji hiyo kesho, mchezo utakaofanyika katika dimba la jamuhuri jijini Dodoma majira ya saa kumi kamili jioni,je wataibuka kidedea hiyo kesho na kuwafikia wapinzani wao Dar es salaam Young Africa?
MKUDE KUREJEA KUNDINI MSIMBAZI.
Mchezaji wa timu ya simba Jonas Jerad Mkude arejea kwenye kambi ya wekundu wa msimbazi Simba baada ya kuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja , kwa kosa la utomvu wa nidhamu.Mkude amewaomba msamaha wadau wote , uongozi wa simba na wachezaji wenzake wote, bila kusahau mashabiki wa simba sports club, nilikosea na sinta rudia tena kosa hilo.kiungo huyo wa katikati wa simba akanusha .na kuomba watanzania wamsamehe kwa kosa lake hilo kwa moyo mkunjufu.
YANGA YAPOKEA NAKALA YA UTHIBITISHO KUTOKA FIFA.
Uongozi wa Dar es salaam Young African umethibitisha kupokea nakala ya hukumu kutoka shirikisho la mpira duniani FIFA yenye agizo la kulipa stahiki za mchezaji wao wa zamani Hamiss Tambwe, pamoja na maelekezo ya kupewa adhabu ya kufungiwa kufanya usajili endapo club itashindwa kufanya hivyo.....
Uongozi wa timu hiyo pia umesema kuwa kucheleweshwa kwa malipo ya mchezaji huyo kumetokana na swala hilo kupitia kwenye ngazi mbalimbali za kimichezo hapa ulimwenguni...
SIMBA SPORTS CLUB YAENDELEZA KIPIGO DHIDI YA DODOMA JIJI.
Clabu ya simba yaendeleza kipigo dhidi ya Dodoma jiji hii leo mchezo uliochezwa katika uwanja wa jamuhuri jijini humo.. Magoli mawili ya MK 14 pamoja na BM3 yatosha kuipa timu iyo ushindi na kuwasogelea wapinzani wao Dar es salaam young African, ikiwa timu ya simba kuwa nyuma kwa jumla ya points 6 tu kuwafikia yanga.
Magoli ya simba yamefunwa na wachezaji Meddie Kagere kunako dakika ya 29 tu ya mchezo, na Bernard Morryson kunako dakika ya 66 ya mchezo. Katika mchezo huo simba walishinda goli mbili kwa moja. (2-1).
MASON MOUNT ACHAGULIWA MCHEZAJI BORA.
Mchezaji wa Chelsea the blues Mason Mount jana amechaguliwa kuwa mchezaji bora katika mchezo uliochezwa kati ya Chelsea Vs Tothenham sport ambapo timu ya Chelsea ilichomoza na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya wapinzani wao , katika ligi kuu England.
EDEN HAZARDS KUTUA CHELSEA TENA.
Kuna tetesi za za mchezaji wa zamani wa Chelsea EDEN HAZARD kutua tena Stanford brigde baada ya kuonekana akifanya vizuri katika Laliga almaarufu kama Satander. Kocha wa timu iyo amedai kuwa watamchukua chezaji huyo kwa gharama ya E 40-50M.
Je usajili wa mchezaji huyo ukikamilika atasaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya uingereza? Toa maoni yako hapo chini.....!!!!
SIMBA HAWAJAWEZA KUMTUMIA MIQUISSONE VIZURI.
Kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa simba Amri Kiemba amesema Jose Luis Miquissone ndiye mchezaji hatari Zaidi katika kikosi cha simba sports club kuliko mchezaji yeyote yule.
KWA NINI MIQUISSONE NI HATARI ZAIDI?
Kiemba anasema simba bado hawajaweza kumtumia mchezaji MUQUISSONE vizuri katika eneo sahihi, bali wanampa maeneo magumu Zaidi.
Kwa kawaida uwanja una maeneo matatu, eneo la ulinzi, eneo la ushambuliaji na eneo la kiungo kwa maana ya malengo. Ameongeza kuwa kwa mfumo wa simba, Miquissone anapewa majukumu mawili, kwanza ni jukumu la ukabaji, pili jukumu la ushambuliaji. Ameongeza kuwa laity angekuwa na jukumu moja tu kama mchezaji CHAMA uwanjani, basi MIQUISSONE ni mchezaji hatari Zaidi katika kikosi cha simba na angekuwa nafunga kila siku.
Kiemba anaamini majukumu ya CHAMA uwanjani ni machache ukimlinganisha na MIQUISSONE.
CEDRIC KAZE AIPONGEZA SIMBA SPORTS CLUB.
Kocha mkuu wa timu ya Dar young Africa Cedric Kaze ameipongeza timu ya simba sports club kwa hatua waliyoifikia katika ligi ya club bingwa barani Africa .Kocha huyo ameongeza kuwa timu ya simba ina wachezaji wengi wazoefu ukilinganisha na timu zingine hapa nchini Tanzania. Kufika mbali kuanzia hatua ya makundi , robo fainali, nusu fainali, na hata fainali ipo mikononi mwa wachezaji na benchi la ufundi la timu iyo, wakiamua kupambana kweli watafika mbali.
Ni dhahiri kwamba timu iyo kwa sasa hapa Africa mashariki ndiyo timu pekee ambayo ipo kwenye ubora wa aina yake ukilinganisha na timu zingine hapa Africa mashariki.
Cedric Kaze amewapa nafasi Simba kwa kufuzu katika hatua ya robo fainali kama wachezaji watajituma na kupambana kwa ajili ya kutafuta matokeo kwenye mechi za makundi Simba itafika mbali kwenye mashindano hayo.
Pia Kaze ameongeza kwa kuwaomba mashabiki wa timu ya simba pamoja na watanzania wote kwa ujumla kuisapoti timu ya simba inayocheza hatua ya makundi ya klabu bigwa barani Africa, pamoja na Namungo anayecheza kombe la shirikisho barani Africa.
AL AHALY KUCHEZA NA BUYERN MUNICH YA UJERUMANI.
Timu ya Al ahaly ya nchini Misri inatarajia kucheza mchezo wa hatua ya nusu fainali na mabingwa wa ulaya, timu ya Beyern Munich ya ujerumani mchezo unaotarajiwa kuchezwa tarehe 8 February mwaka huu, majira saa 3:00 usiku kwa masaa ya Africa mashariki. Je timu iyo ya afrika watafua dafu kwa mabingwa hao wanaotamba ulaya? Toa maoni yako hapo chini........!
YANGA KUFUNGWA NA TIMU NDOGO.
Dar es salaam Young African ya jangwani imecheza mechi yake ya kirafiki na timu ya African Sports ya jijini Tanga, ambapo katika mchezo huo uliochezwa majira saa 7:00pm usiku, katika uwanja wa Azam complex chamazi jijini Tanga, timu ya African Sports imeibuka kidedea kwa ushindi wa goli moja kwa sifuri,(1-0) bao lililofungwa na mchezaji Uledi dakika ya 74 ya mchezo.
Timu hiyo ya yanga ya Dar es salaam wamepoteza mchezo wao huo muhimu ambapo pia ni maandalizi ya kujipima kwa ajili ya roundi ya pili ya ligi kuu bara . Ikumbukwe kuwa timu ya Yanga ndiyo inayoongoza ligi kuu ya Tanzania bara ikifuatiwa na bigwa mtetezi Simba ya Dar es salaam.
LEO NI SIMBA NA AZAM .
Timu ya Simba Sports Club inatarajiwa kushuka uwanjani kucheza na timu ya Azam katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam majira ya saa kumi kamili jioni, ikiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Timu iyo inacheza mchezo wake ambao ilishindwa kucheza kwa sababu ya mashindano ya klabu bingwa barani Africa.
Mabingwa hao baada ya mchezo wao dhidi ya timu ya Azam watalazimika kusafiri hadi nchini Congo tayari kwa mchezo wao mwingine katika hatua ya makundi, simba wataanzia ugenini, na kumalizia nyumbani dhidi ya As Vita Club ya Congo.
SIMBA NA AZAM WATOKA SULUHU VPL.
Wekundu wa msimbazi simba sports club wametoka sare ya goli mbili kwa mbili dhidi ya Azam , mchezo uliochezwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam majira ya saa kumi kamili jioni.
Katika mchezo huo timu ya Simba ilionekana kumiliki mchezo na kuliandama lango la wapinzani wao Azam Sports club na kufanikiwa kupata goli la kuongoza lililofunga na mshambuliaji mahiri na matata, anayefahamika kwa jina la Bull striker, hapa namzungumzia MK. 14 ambaye alilitumia vyema krosi ya mchezaji matata uwanjani Luis Jose Miquissone na kuimalizia nyavuni. Baada ya mapunziko kipindi cha pili timu ya Azam kilibadilika na kuanza kucheza mpira bila kujali chochota, hatimaye ilifanikiwa kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao mahiri Iddy Suleiman ambaye alipiga shuti kali kwenye Angle ambayo Aish Salum Manula hakuweza kuicheza hivyo kuifanya timu iyo kupata nguvu na kurejea mchezoni kwa ari mpya.
Mshambuliaji huyo hatari wa timu ya Azam Sports club aliwanyanyua tena mashabiki wa Azam Sports Club baada ya kuwafungia bao la pili ikiwa ni kipindi cha lala salama , au lala kwa buriani, na kuifanya Azam kuongoza mchezo huo.Timu ya Simba ilifanikiwa kusawazisha goli la pili kwa kupitia kwa mchezaji wao kutoka Msumbiji Luis Jose Miquissone hivyo matokeo kuwa sare ya goli mbili kwa mbili.
MANARA ASAFIRI NA TIMU YA SIMBA CONGO.
Msemaji wa klabu ya wekundu wa msimbazi Simba Sports club amesafiri pamoja na timu nzima ya wekundu wa msimbazi simba kwenda nchini DRC CONGO kwenye mchezo wao muuhimu dhidi ya timu ya AS VITA CLUB, mchezo unaotarajiwa kupigwa siku ya ijumaa majira ya saa mbili kamili usiku kwa majira ya Africa mashariki.
Zanzibar Broardcasting channel itakuletea huduma hiyo live kutoka Congo kishansa nchini Congo. Kumekuwa na maswali mengi sana mitandaoni ambapo mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania na nje ya Tanzania wakiwa nanahoji kuwa ,timu ya Simba sports club watafua dafu dhidi ya AS ITACLUB maana mwakajuzi timu hiyo ya Congo walichuana na Simba sports club vikali hatimayee, Simba ya Tanzania walifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya Robo fainali ya club bingwa barani Africa.
Post a Comment